1. Jijini Dar
chorus
Misele ya Kinondoni, ya Temeke, ya Ilala
Jijini Dar-es-Salaam
Nikakatizia Tanga, Mwanza, Kigoma, Tabora nikarudi
Jijini Dar-es-Salaam
Kona za Buguruni, Kariakoo, mpaka Posta
Jijini Dar-es-Salaam
Nikakatizia Zenji, Mombasa, Kampala, Kapirimposhi nikarudi
Jijini Dar-es-Salaam
Misele ya Mwananyamala, ya Manzese na Ubungo
Jijini Dar-es-Salaam
Nimefika mpaka China, Urusi, Ujerumani, Marekani nikarudi
Jijini Dar-es-Salaam
Mimi ni msafiri bado niko njiani, ninakokwenda nitafika maana ninakujua

Verse 1
Tangu sabini na nane, usiku wa manane
Darda King nilishuka ulimwenguni nimenyane
Muumba aliniambia dunia ina mwenyewe
Ukipita salama, thawabu yako itakuwa nawe
Barabara kuu ya hali ngumu na mvua ya mawe
Ni heri vyenye mabawa virukavyo kama mwewe
Utajiri utamchagua nani kati ya mimi na wewe aah!
Mzichi! asiye na mwana aeleke jiwe
Mfalme ni Mfalme himayani kwangu nitawale
Nina mabingwa wa sanaa maonyesho na vitendo tele
Usilete za kuleta na hadithi za Kalumakenge
Wanahanya wapate menyu Mazichi wana unenge
Miaka ya themanini wacha hisia zitupagae
Wasanii walipotajwa kama Sikinde ngoma ya ukae
Kwenye tisini feni likapepea mbele
Miondoko ya kikongo ilipodundwa na Kabasele
Karne ya ishirini na moja nakuja kama mpira wa kona
Wanakuja kichwa kichwa babu sijapata kuona
Duniani Darda King mimi ni bado msafiri
Popote nitokeako mazichi mnipokee
Repeat chorus

Verse 2
Masafa ya ndani na nje, ki Vasco da Gama
Farasi alipogoma mi kwa ngondi nilichoma
Some times nikala boda kwa boda kama Osama
Dunia nzima nakumbushia Hiroshima
Mabibi na mabwana amini tu ninachosema
Nimekutana na watu mashuhuri tena noma
Nelson Mandela mzee wa heshima
Dunia nzima imempatia vema
Mu'Ammar Gadafi mzee wa mitikasi,
Fidel Castro kila dakika yuko wima
Wasanii wa muziki wakali waliovuma
Mos Def, Hide wa Japan, Remmy wa Matimila
Wana masumbwi wagumu kama chuma
Tyson, Isangura nao wakina Matumula
Wanakabumbu vinara waliojituma
Makumbi Juma, Malota Soma, Gaga na Kihwelu Musa
Mwanakikapu hatari niliyemwita MJ
Akitisha akiruka kimetinga
Duniani Darda King mimi ni bado Msafiri
Popote nitokeako Mazichi mnipokee
Repeat chorus

2.Kanazi
Chorus
Hivyo ndivyo vituko vya mtaa wa Kanazi
Watoto wanacheza
Hivyo ndivyo vituko vya mtaa wa Kanazi
Wengine wanalia
Hivyo ndivyo vituko vya mtaa wa Kanazi
Oya! bingwa umeiona hiyoo
Hivyo ndivyo vituko vya mtaa wa Kanazi

Verse 1
Nyumba namba saba mtaa wa kanazi
Ndipo walipokuwa wanaminya wakimbizi
Miaka sita saba wakatuachia sisi
Banda la uwani nikawa napigia ndizi, Mzichi
Sasa nimeshaota mizizi
Mtaani ni kama nahodha wa jahazi
Wacha nimzukie Suzi
Hapa geto ninaona mambo gozigozi
Naingia mtaani, watoto kwa wazee wananipigia pozi
Vijana wana bling rangi zao za mavazi
Mademu wame chill wanajisikia luuziii
Bado nawavutia pumzi
Najua siku moja nitapata mapenzi
Dukani nikapate mbili dozi
Kisha nizunguke nikamwone Babu chizi
Kugeuka wanamkimbiza mwizi
Mshike mshike wakampiga kitanzi
Wakati Pafi kazunguka kusaka kazi
Pati twenty four anadunda tumbo wazi
Wakatu Shubi yuko chuo kwenye kozi
Bado mama Chuki ana supply maandazi
Ya leo babu kubwa, cha mtoto ya juzi
Huo ndio msemo wa mtaa wa Kanazi

Repeat chorus

Verse 2
Kanisa la Kibatisti kwa nyuma kuna uwazi
Ndipo Liver Pool wanapopigia tizi
Japo kuna visiki na magoli ya miti
Mazichi kila jioni wana lisukuma gozi
Siku ya mechi kali wote wana jezi
Refa ni mvinje bwana hataki ushenzi
Leta za kuleta utateguliwa tezi
Jebu kali mpaka ubongo utakufa ganzi
Edi Baba anakaanga viazi
Mama ntilie anachachua mchuzi
Seremala anakusanya vibanzi
Watoto wa mama Roda bado wanadaka panzi
Anti Juli shoga yake na Nazizi
Yuko kichochoroni analichunua buzi
Baba anambatua mama Nyamizi
Amemfumania na Chale muuza nazi
Jamila macho yanamtoka machozi
Ameshapewa mimba na mjumbe wa nyumba kumi
Bora nikajichanganye vijana jazz
Kusiko na mabraza-meni ambao hawa chezi
Ya leo babu kubwa, cha mtoto ya juzi
Huo ndio msemo wa mtaa wa Kanazi
Ya leo babu kubwa, cha mtoto ya juzi
Huo ndio msemo wa mtaa wa kanazi

3 Tulingeba
Intro
Astaghafiru-llah, Nimerudi Darda King
Mfalme mwenye hekima na maarifa
Napenda kuchukua nafasi hii
Kuitambulisha miondoko ya Tulingeba
Ulimwenguni kote, kutoka Dar-es-Salaam

Wakina mama kedekede naona wanayo hamu
Wanakatika wakisikilizia utamu
Morani matumbo wazi long time
Wanaruka juu na kutua kwa zamu zamu
Chezeni pamoja wote binadamu
Kata mauno mpaka chini chamgamsha damu
Oya! Mzichi mbona hauchezi?
Ah! Darda King nataka cheza bila Demu!
Ninakuja nayo midundo ya tulingeba
Imeshashika chati kama banchikicha
Huko Beijing wananiambia shieh shieh
Jamaica wananipa ya-man!
Amerika wamebaki midomo wazi
Afrika nasikia wananchi hawalali
Mazichi wangu mabibi na mabwana
Viuno legeza tucheze tulingeba

(Tulingeba yoyo)x3 tulingeba
Tunakuomba wewe dada uje hapa
Tukuone maringo yako, maringo yako
{(bingiri)x5 mpaka chini} x8

(Tulingeba yoyo) x3 tulingeba
Tunakuomba wewe kaka uje hapa
Tukuone maringo yako, maringo yako
{(bingiri)x5 mpaka chini} x8
Ah! wacha bwana, Darda King
Midundo live, Houston Texas represent Bongo

4. Zaburi 23
Intro
Naam, nijapopita katika bonde la uvuli wa mauti
Sitaogopa mabaya maana Wewe upo pamoja nami
Gongo lako na fimbo yako vyanifariji

Verse I
Sidhani kama nina tena mpinzani
Maana peke yangu Mfalme nimebaki
Na hata kama kuna wanaotaka upinzani
Mpaka nikiondoka vijakazi watabaki
Na kila mimi nilalapo kitandani
Maono ninaona ya wanao nidhihaki
Na kila mimi nisimamapo jukwaani
Furaha naleta kwa wapendao burudani
Naona wapo wanaotaka ushindani
Mimi ni Mfalme wafuasi watabaki
Ee Bwana, kama wametoka Ushenzini
Waeleze Dardanus ni Mfalme aliyebaki
Na kila Darda King nikaapo enzini
Milango nafungua kwa wanaotenda haki
Na kila Darda King niwapo mikasini
Ni mishindo ya kushindua kama mkuki
Amini chochote kinitokacho kinywani
Maana siwezi kukwambia nisichojua
Jua linapokuwa kali napiga miwani
Kofia ya bazuka inaponyesha mvua
Moshi wa mjani uko hewani
Hatua mbili mbele tatu nyuma mchoroni
Na mijicho myekundu mitaani
Vichochoro nikunje nitokee Kinondoni
Afande akizuum ninunue pikipiki
Vikinishinda nivitupie machakani
Nikimtoka nipige misele miwili
Niruke ukuta niibukie maskani
(Nilishaumwa na nyoka, nikiona unyasi ninashituka
Nilishakubwa na dhoruba, na bado baharini mimi nitavuka)x2

(Hakika wema na fadhili zitanifuata
Siku zote za maisha ya Darda King)x6

Verse 2
Nasikia wapo wanaonong'onanong'ona
Wanaosema mimi ni Mfalme gani
Nasikia wapo wanaotokotatokota
Chora michoro kuniweka kizuizini
Nipeleke kwa pilato ukidhani nina kosa
Nitalipa akinishika na hatia
Amenawa na amesema sina makosa
Amesuuza mikono, sina hatia
Ushahidi wa makosa mkikosa
Ya bandia mwaanza nibandikia
Wapambe nuksi nasema sina makosa
Ya nini mabango mnanishikia
Joho langu linang'ara kwa weupe
Mbona madoa mnataka kulitia
Kitabu changu kina kurasa nyeupe
Mbona madhambi mnakiandikia
Mimi ni Mfalme mwenye hekima
Nilikuwepo nipo na bado nitakuwepo
Mimi ni kama yule Msamaria mwema
Nilikubeba walipopita kama upepo
Mazichi wote duniani wamenikubali
Tangu nilipokuja na nani kama mama
Huko kwa Kibaki mimi ni kama almasi
Tangu nilipodunda midundo ya Nairobi
Mwanaume maneno naweka kando
Na kama nikisema ujue kuna vitendo
Nimeamua niwe kama kondoo
Nimeshamaliza lakini mambo bado
(Nilishaumwa na nyoka, nikiona unyasi ninashituka
Nilishakubwa na dhoruba, na bado baharini mimi nitavuka)x2

5. Kaburu
Ye ye ye yea, Darda King, Kaburu
Ndani ya nyumba, hakuna shaka kata shingo
Mfua chuma pata shika, seke seke
Mwaga majalo kama Yanga na Simba
Mpira kati tupa kitu, huyu Kaburu
kuwa makini kama hivi
Utangulizi umenielewa mimi ni nani
Sina utani Kaburu napora pipi kwa mtoto
Chezee moto wa tipa nakupa kubwa
Kuwa mbishi utapigwa ndizi
Maji ya shingo toka mbio
Hii ni fani nyingine bwana mbali na kazi
Kula bia, pata mjani, kula chaki na shika mic
Mwaga radhi, hizi raba nyingine
Kama hivi kama vile, mimi na Darda
Nagonga hodi, (bom)x3 ndani ya Bronco mpaka bongo
Kata nyodo, watoto oo ooh Kaburu amekita mjini
Hapakaliki mbindembinde mshikemshike
Wanoko mpishe nakupa misheni
Pata fuba zungusha kamata nyumba 745
Funga mguu 23 kama babu wape tabu
Waliokuona wewe ni kavu, wanalia chumvi
Wanakula vumbi kushoto kulia tupige bia
Hamna vita, dili limeitika msela kashinda
Machoko mjini mmekwisha

6. YiHo!!!
(YiHo!!! YiHo!!!)x2

Verse1
Kama una ki-blauzi kipige mkunjo
Piga machejo onyesha manjonjo
Kama ni khanga moja nipigie fundo
Kwenye ki-sketi kata mauno
Shega shega tingisha mabega
Shika kamata kama ni ya moto mwaga
Saga saga rumba mpaka majogoo
Msaada kwenye tuta, sooo
Mazichi wanayumbayumba na kujigusagusa
Pa jipangusangusa kwa jikwaruzaruza
Wanaburudikadika kwa kujirusharusha
Kisha wanasema hiyo ni safi safi
Kila mtu na demu wake fakdat
Babu yangu kamata wawili
Naona mambo yamenoga waa waaat
Ona wanavyonipigia makofi
Mademu wanashushashusha na kubinukanuka
Sha jishanuanua, re jirembuambua
Wanajisikiakia kwa kujishikashika
Kisha wanasema Darda King
Wanataka niwapakate
Tugandane kama siagi na mkate
Wanataka niwape mate
Mazichi wananipigia makofi

Chorus
(Ninaimba verse Imbeni kiitikio YiHo!!! YiHo!!!)x2
YiHo!!! vimwana tingisheni makalio YiHo!!! YiHo!!!
YiHo!!! mazichi zungusheni visigino YiHo!!! YiHo!!!

Verse 2
Kama una manoti nyanyua mikono
Zungumza kwa pesa na sio mdomo
Mapigo babu kubwa pasipo mfano
Kuanzia Alhamisi mpaka Jumatano
Vunja mifupa wakati una meno
Yakibaki mapengo fungua mabano
Ukiwa arosto tuliza mshono
Potelea mbali wakitutolea mfano
Kama una mkoko weka mikono juu sema YiHo!!!
Kama unalo geto weka mikono juu sema YiHo!!!
Kama hauna demu weka mikono juu sema YiHo!!!
Kama hauna meni weka mikono juu sema YiHo!!!
Kama unapuliza weka moto juu
kimbiza mwenge uweke kuleleni juu
Kama ni wa mitungi tuone chupa juu
Kisimu cha mkononi nacho kiweke juu
Ukipagawa njoo hapa juu
Kapelo yako iweke juu
Ukinogewa njoo hapa juu
Na hilo shati lako nalo liweke juu

Repeat chorus

7. Mjani
Chorus
Zungusha mjani chupa za kijani
Kisha nipe na mzinga wa konyagi
Zungusha mjani chupa za kijani
Nipatie na mzinga wa konyagi
Zungusha mjani digida kijani
Kisha nipe na mzinga wa konyagi
Zungusha mjani moshi hewani
Tulizia na mzinga wa konyagi

Verse1
Kila tunapojificha kijiweni
Ujue hali ni ngumu duniani
Tunawaza na fikiri kwa makini
Kuongezea mali tufanye nini
Ishirini iwe arobaini
Ongeza thelathini iwe sabini
Tujivinjari kama madingi zetu
Walivyotesa miaka ya sitini
Ndio maana hatutaki mademu
Sababu kuepuka mambo kisebusebu
Tokeni zenu dunia ya sasa
Ni bora nimpende ndugu yangu wa damu
Wanakuja kamavile wagonjwa
Wanavyokimbilia kumuona mkunga
Alright mimi dozi nawapa
Ikishawaingia fresh, please timuka
Tumechunguza tumegundua
Mademu wengi wanapenda kuchuna
E bwana tumeshituka
Ndio maana tunawapiga bunda
Kwa mazichi imani nimeweka
Kwani walinibeba nilipopiga mwereka
Rumande walinitoa
Na sasa tuko mtaani tunaserereka
Asubuhi tunatafuta pesa
Mchana msaada kwenye tuta
Adhuhuri tunatumbua pesa
Usiku mambo ni kutwanga na kupeta
Karibuni Kijiweni vitu vinakopimwa bila mzani
Paf paf paf kisha pasi
Suuzia na mzinga wa konyagi

Repeat chorus

Verse2
Aste aste ndio mwendo wa mazichi
Na menyu yetu ni bondo kwa kabichi
Nipe ule mzinga mkubwa wa konyagi
Nitaumaliza kabla ya saa kumi na mbili
Moshi unafuka mazichi tumewaka
Tunapayuka kama daewaka
Mimacho myekundu kama vile paka
Ukitukasirisha sisi bado tunacheka
Cheka cheka kama babu Mahoka
Lakini moyoni kama simba wa nyika
Ee bwana tukikasirika
Tunakuja kama mvua za masika
Na kama usipotupisha
Tutakukumba uvunjike mshipa
Ulishashauriwa kama kipipa
Ujiepushe na anasa za dunia
Ufikirie maisha ya baadaye
Mh Ukasema labda baadaye
Unajuta, jijutie
Maneno ya wahenga uyasikie
Unalia, jililie
Mapigo ya Mazichi uyanyatie
Tunaibuka na sura mpya
Tunapanda juu chini hatutoshuka
Tunafoka sauti mpya
Za kususuza kama Bitchuka
Mwaka mpya, mitindo mipya
Kamavile tumepandisha mzuka
Njooni kijiweni
Maraha yanarahwa bila ugomvi
Paf paf paf kisha pasi
Suuzia na mzinga wa konyagi

Repeat chorus

8. Elimu Afrika k.k.n. Eaze
Chorus
Mwanafunzi wa Afrika kichwa ngumu
Ana mambo milioni kichwani
Mwanafunzi wa Afrika kichwa ngumu
Ana vitabu mia mgongoni
Mwanafunzi wa Afrika kichwa ngumu
Ana shilingi sabini mfukoni
Mwanafunzi wa Afrika kichwa ngumu
Ana njaa babu kubwa tumboni

Verse 1
Maisha ya Mwanafunzi Afrika Mazee ni wazimu
System demokrasia kufukuzia matumbo yao
Huku shuleni sina mwalimu
Ikabidi ni change life penda sana kula ndumu
Huku shuleni everybody tough on you
Likizo ikafika alright see ya! naona soo kurudi home
Juu Mbuyu wangu ata coz
Results zangu sina A sina B sina hata C
Zote F mazee acha nikakaba mpaka mashingo
Nikafukuzia madili mpaka pale street
Ala what i didn't give nothing but shit
Next time ikabidi ni fall down to my knees
Omba Mola mazee if you want to succeed
In anythig Waafrika wote ninawasihi
Kutoka kindergarten mpaka universiry

Repeat chorus

Verse 2
Shati ni jeupe na kikaptura cha bluu msingi
Mpaka nikakivuka kigingi
Kuingia secondari nikawa kibonge cha kidingi
Na mambo yangu yakawa yanakwenda kidingidingi
Ee bwana babu yangu nikawa na washikaji wengi
Wengine wasongo na wengine wavuta bangi
Na demu mmoja tu wengine ni mashangingi
Lakini kila wikiendi nafikiria mitungi
Makonda wanaleta ninawapa tu masumbwi
Varangati kali ah! naishia polisi posti
Kurudi shuleni nimepigwa suspension
Potelea mbali nitajidunga tu ma-twisheni
Walimu staff room wanafikiria pensheni
Wanafunzi darasani wanafikiria feki
Monita niandikie majina ya wanaopiga kelele
Nakwenda wizarani kufuatilia cheki
Na mwisho wa wiki hii kuna mtihani
Anayetaka msaada wa karibu nione ofisini.

Repeat chorus

9. Simu

"Answering machine" (Interlude)

10. Ulivyotaka k.k.n Shanita
Chorus
(Ndivyo ulivyotaka aaa)x4

Verse 1
Miezi kumi na mbili,tangu tulipofunga ndoa
Na harusi ya kishua,kama queen nilijisikia
Nilichotaka Darda ulinipa, nilipolia ulinibembeleza
Kimapenzi kwako nilifika, kimahaba kwako nilikita
Nikajaambiwa kususu mashuga mami
Wanao kuhudumia , ukanikatalia
Nikaletewa na picha, za yule nyumba ndogo
Unayetangazia, mmh! ukaguna
Nikajasikia kuhusu viruka njia
Vinavyokuvizia, ukanibishia
Ya mwongo ni fupi njia
Umeficha moto moshi umekuumbua
Una watoto kila njia
Umekuwa mbwa mwitu aliyejivisha ngozi ya punda milia
Umekuwa kama chatu unanikamua kila siku ninalia
Na mengi zaidi ya hayo, mwenzako nilivumilia
Hata uliponitukana, bado nilivumilia
Na leo ndio mwisho, ndoa yetu hapa imefika mwisho
Chini ya kitanda changu chumbani kwangu
Chupi na sidiria visivyo vyangu
Naleo ndio mwisho, ndoa yetu hapa imefika mwisho
Sitaki yako maelezo, ndivyo ulivyotaka aaa

Verse 2
Mke wangu tafadhali tena nakusihi
Maamuzi ya haraka sio sahihi
Mume wako sheli bado ninakujali
Nipo duniani mimi sio kamili
Watoto wanatuhitaji kuyakidhi yao mahitaji
Na Mazichi wangu kama R.Mataji
Wanajua wewe ndio wangu gwiji
Sabuni ya Roho wangu una ufunguo wa moyo wangu
Mapigo ya moyo wangu, ukiniacha ooh!
Nilihadaika na anasa za dunia
Nikashawishika na mvuto wa vinasa
Nilidanganyika kwa utamu wa kashata
Kahawa ilipokuja mimi bado nimenasa
Mpenzi naomba nipe tabasamu
Ingawa tuko uzunguni tumetoka Dar-es-Salaam
Kinondoni, Ilala, Temeke, ni maisha ya kizichi
Na mila za kizaramo, ni maisha kamarachi
(Nina mpango, poa kidogo, nikupeleke migomigo
Tukamalize, chokochoko, hiki kilio kiwe kicheko) x2

Repeat chorus

11. Nimekubali k.k.n.Tasha
Chorus
(Do what you want pa have it your way
Do what you want ma have it your way
Do what you want pa have it your way, my lady) x2

(Hey pa, nimekubali x3 nimekubali
Hey ma, nimekubali x3 nimekubali) x2

Verse 1
Nimekubali hakuna matata
Have it your way no worries my Darda
You're the only papa that makes me holla
Im stuck on your love like Ringo Manticala
Hakuna matata, i'll never hurt ya
Pac is on low mama never desert ya
Sickness and health tear death to a spot to abortion
Lite a light after dark
Promise to play my part, nimekubali Darda
From finish to the start, they can't separate us nada
Me without you, i beg my pardon
Your love is at you risk like Osama bin Ladan

Repeat chorus

Verse 2
Sikio la kufa mami halisikii
Dawa na hata ganzi haviingii
Pale moyo unapodunda kimapenzi
Mahaba yanapogeuka maradhi
Nafanya ninavyotaka mani bila shaka
Nakwambia ninacho feel honey sina noma
Unaona ninavyobling sweetey, kama nyota
Halafu cheki ninavyo bling shorty
Ninajituama ifikapo ijumaa
Kwani najua nyumbani kwangu utajaa
Mzichi nakuwashia mishumaa
Kiufundi kwa chati taap ninazima taa
Mapenzi yetu tumeyapeleka mbio
Wengine tumewapiga kisigino
Najilikia kama nimeshinda bingo
Kila ninachosema, umekubali

Repeat chorus

12. Umeniacha
Chorus
Nimejibanza, kichakani kwa sababu umeniacha
Naweweseka, vitani peke yangu umeniacha
Nahuzunika, nashika shavu sababa umeniacha
Nafarijika, najua siku moja tutaonana
Nimejibanza, kichakani kwa sababu umeniacha
Naweweseka, vitani peke yangu umeniacha
Nahuzunika, nashika shavu sababa umeniacha
Nafarijika, najua kwa Muumba tutakutana

Machozi bado yananitiririka, kila mara ninapokurikiria
Nimepiga ukuta na kuvunja vioo,
Lakini uchungu moyoni hauishi oh
Nimemuuliza Muumba ni kwa nini oh
Amekuondoa mapema duniani oh
Wakina mama wamelia kilio
Kina shangazi wakalia kilio
Kina dada walipoimba pambio
Kina baba wakaimba kiitikio
Umeniacha Mtilio, ni mateso makali sana moyoni oh
Nakumbuka enzi za kiskio po!
Hata enzi za mchezo wa kidali po
Nakumbuka zile enzi za skuli oh
Uliponishika mkono kuvuka streets oh
Maisha kwangu yalikuwa malaini oh
Nilikuwa tu nafuata nyayo zako
Nitafakaripo naiona sura yako
Upumzike kwa Amani milele oh.

Repeat chorus

Verse 2
Nafsini mwangu nina mahuzuniko
Akilini mwangu nina michanganyiko
Ndugu jamaa na wote rafiki zao
Usiku na mchana wana maombolezo
Junior wala haelewi aonacho
Mimi naona ni kama kiini macho
Nilisimama wima nikararua joho
Nikaanguka chini kwa kifudifudi oh
Chakula nakitazama na wala sili oh
Vimiminika kwenye koo havipiti oh
Kila ninachofanya naona kama sio
Shughuli zote hamsini hamsini oh
Kitanda chumbani hakilaliki oh
Nimejaribu vingi pasi mafanikio
Maisha kwangu yamekuwa ni magumu oh
Inanibidi niushike usukanio
Nitafakaripo nahisi kicheko chako
Upumzike kwa Amani, milele oh

Repeat chorus
Inna Lill La-hi wa-Inna, Ill-Lahi raajiuun

 

 

 
Home  |  Media  |  Events  |  Photo  |  Contacts
Copyright © 2003 - 2007 Mfalme  |  Privacy Policy
n