Nimeshinda 2007

1. Jiwe
Chorus
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na wapambe nuksi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na redio za kuni,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na wazakinabinabi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na wapenda khaki,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,

Verse1
Manying'inying'i yo!, roho za kwanini yo!,
Kifuniko shaba hayo yote ni ya nini yo!,
Kono la bao yo!, macho ya paka yo!,
Kizingiti chuma unanitakia nini yo!,
Ulinikandia, ukanizibia yo!,
Ukaniangusha nikadunda kama kitenesi yo!,
Ukanichambua, ukanichekecha,
Chekechoni sikupita mzichi nimenawiri yo!,
Nimeona dira sasa, na muelekeo,
Nimeshinda KO umezira kula ni kwa nini yo!,
Ulikomalia vijarida vinichore kikatuni,
Kikatuni kikageuka Mfalme wa vikatuni,
Ulipakazia paka kashfa majungu gunia,
Jiulize mara mbilimbili wapi nimekukosea,
Nimepangakuni safi na moto nimechochea,
Mfalme nimekubalika uliza dunia nzima,

Chorus
Nilikataliwa na wapambe nuksi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na redio za kuni,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na wazakinabinabi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Nilikataliwa na wapenda khaki,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,
Jiwe walilolikataa waashi,
Nimekuwa Jiwe kuu la pembeni,

Verse2
Kisebusebu yo!, na kiroho papo yo!
Mbona unabisha bado mimi ni mshindi yo!
Wamekuhakikishia, kwenye top ten show,
Mbona hautaki bado mimi ni zaidi yo!,
Pilipili tulivu bado iko shambani,
Huko sokoni inakuwashia nini yo!,
Mti mkavu babu, hauchumwi dawa no,
Nenda katambike kwenu, mimi ni kinara yo!,
Zinafagiliwa na mazichi tungo za mistari yangu,
Sikiliza na midundo  yake bado ni stereo,
Imepaliliwa na kuwekewa mbolea kazi yangu,
Sikiliza na sauti yangu bado ni mchicha yo!,
Kama vitani mimi ndio top Jemedari,
Kwenye karateka mimi ni kama vile Shikoshugi,
Wanatumiwa na mashetani hadharani,
Wanaoonyesha kwa kidole cha katikati,

Repeat chorus


2.Uhai
Chorus
Uhai x2
Najua utajinyima vingi,
Na mwisho wake kuna maumivu makali,
Miezi tisa nakuomba nivumilie, nisaidie,
Unilinde tumboni nipatie nafasi……Uhai
Najua wengi watakusema,
Kuna watakaothubutu kukuita kahaba,
Miezi tisa nakuomba nivumilie, nisaidie,
Unilinde tumboni nipatie nafasi,……Uhai x2

Verse1
Naomba tufunge safari ya hospitali,
Daktari akajue nina hali gani,
Kama mbali nipeleke hata ki-kliniki,
Waone nimegeukia upande gani,
Ngumi zangu nimekunja macho yangu nimefunga,
Moyo wangu unadunda ndio maana nimejikunyata,
Nasikia, maneno wanayokuambia,
Tumaini langu ni uamuzi gain utafanya,
Nasikia wote, wanaokuambia toa mimba,
Hali yenyewe ngumu na chakula ni cha shida,
Nasikia wote, wanaokuambia toa mimba,
Shule hujamaliza aibu kwa familia,
Niruhusu nije duniani ma nitawasalimia,
Hatakama ni mimi na wewe tu mi nitavumilia,
Kila ninavyokua kwa Mungu ninakuombea,
Nisaidie miezi tisa naomba nipiganie,

Chorus

Verse2
Sigara  unazovuta mama zinaniumiza,
Hewa unayovuta ndio mimi , ninategemea,
Na pombe unazokunywa mama, zinanimaliza,
Sina pa kukimbilia naomba nifikirie,
Huwa nasikitika wanapokusikitisha,
Huwa nasononeka wanapokusononesha,
Natabasamu nikisikia unacheka,
Napata usingizi safi unapokuwa na furaha,
Usifanye kazi nyingi sana, nipumzishe,
Nimechoka kujigongagonga shingo yangu inauma,
Nivumilie usimbufu ninaokupa,
Kichefuchefu kutapika na homa za kila mara,
Nimekusababishia kizunguzungu,
Umelala chini umejikuta chini ya uvungu,
Wapambe nuksi bado wanakupiga majungu,
Nivumilie miezi tisa naomba nipiganie,

Chorus
Mama naomba unipe nafasi, unajua naweza kuwa
Raisi wa nchi, kiongozi wa dini, mwalimu,
Ninachoomba ni nafasi tu

i
3 Tayaribado
Ah! Lion 808
Chorus
{Tayaribado?   Bado!
Tayaribado?  Aahh!} x4

Verse1
Kwenye dance floor nenda kajifiche,
Nikutafute na nikukimbize na nikikushika pah!
Nikudalike, ukigeuka kiuno nikukamate,
Mchakamchaka cha! tuchekechane,
Kizunguzungu zu, tuzungurushane,
Kwa leo usiku tusipoteane,
Tukipoteana basi tutafutane
Tayaribado nimeuliza, mtoto mzuri bado ukaitika
Lakini mzichi subira imenitoka
Natakashika kinachotingishika,
Tingisha tingisha, kisha shituka
Mtoto wa kibongo onyesha unavyokatika,
Chekecha chekecha, kisha binuka,
Teremka chini tuone unavyonengua,
Nimedata unavyotingisha kishumizi,
Imenibidi mwa nipige mbizi,
Kimwana hebu niplizi, nikuplizi,
Kisha niyakidhi yako matumizi,
Siongelei habari za uzinzi,
Nafikiria uwe wangu msaidizi,
Ila tu Usinifanye buzi,
Elewa somo ingia kwenye jahazi,

Chorus
{Teremuka x4 chekecha x4} x2
Chorus

Verse2
Unavyotingisha, Unavyochekecha
Sina la kusema mami unapendeza,
Unavyoonyesha machejo yasiyochojeka
Wenye roho nyepesi kinoma wanateseka
Naona mabronzo wanavyokuwinda,
Kwa magobole wameshakulenga,
Mwingine anakwambia nina pese,
Mwingine anakwambia nina lexus,
We mtoto kumbe hubabaiki
Kwa herufi ndogo kumbe hauambiliki,
Kwa kuchekecha kumbe hautaki,
Lugha ya vitendo hawa ieleweki,
Tayaribado nimeuliza, mtoto mzuri yes umeitika
Kiminyato ninakusogelea,
Kimapozi ninakukamatia
NImekonyeza, ukacheka, nikavuta, ukavutika
Nikabamba, ukabambika, nika kat kat, ukakatika
Lugha ya vitendo ndio inatawala,
Pesa zako weka mfukoni,
Ubrazameni weka kibindoni
Ingia kwenye dance floor cheza mpaka monie,

Chorus
{Teremuka x4 chekecha x4} x2

Chorus


4. Cowboy
Chorus
Mimi ni real real cowboy x4

Verse1
Mimi ndimi mzichi slash cowboy,
Wapambe nuksi slash haters wako hoi,
Hoi wanavyobanwa na kikohozi,
Mademu wanaponiita cute boy,
Wanapenda ninavyo move kimahaba,
Wanapenda ninavyotema bongoflava,
Midundo toka bara mpaka pwani heavy duty
Inakita ngoma za masikioni,
Mwanaume wa shoka kibindoni nina shoka
Hata uwe kama mbuyu nadondosha,
Nini nilikotoka cheki ninakokwenda
Uswahilini uzunguni nimelikita,
Waliojidai namba moja wameshika,
Wamefurukuta mpaka wamechoka,
Mzee nikitupa ndoano hata bila ya chambo,
Samaki wanagombania kwa vikumbo,
Waliosema kileleni sitofika
Wamebwajabwaja sasa wako hoi,
Babu nikiwa jukwaani hata bila ya maiki
Wananishangilia like …….

Chorus

Verse2
Hivi umekicheki kiatu changu
Umelicheki jinzi langu,
Umelicheki kapelo langu
Babu hebu kong’otea shati langu,
Utazimika na mwendo wangu,
Utalipenda pozi langu
Bado sijakuonyesha machejo yangu
Ninapokuwa juu ya farasi wangu,
Mimi ndimi championi wa rodeo
Kama huamini nicheki kwenye video
Na muziki wangu badoni stereo
Kama huelewi daka tafsiri yo!
Waliniambia kutesa ni kwa zamu,
Nikawaambia mh! Mh! Mfalme hana zamu,
Natesa alfa mpaka omega,
Niko juu chum! Kiulaini namega,
Navutia kwangu mambo yote ni shega
Niko full chum!, kiufasaha nalonga,
Kila ninacholonga wanapiga makofi
Wananishangilia like …….

Chorus.


5. Daladala

African public transportation (Interlude)

6. Mdundiko
Chorus
Mtoto wa Kinondoni nimekubalika kama hivi
{Havinitishitishi, eeh!, havinibabaishi, eeh!
Wewe mtoto vipi, eeh!, ule mpango vipi, eeh!} x2

Verse 1
Magoma mazito, ndani yake ni mikiki mizito,
Na vinavyotingishwa ni vizito kwa chikito,
Pokito mchecheto,
Ngoma nzito, inadundwa na misuli mizito,
Inawapagaisha mabitoz na mashitoz
Inaitwa mdundiko,
Maji marefu dandia nanga,
Aste aste usiangushe shanga,
Usione noma, demu akigoma,
Kitimutimu, kisebusebu,
Kifua chini mikono chini, macho juu,
Nikisema wa!, wanasema wamsegeju,
Chekecha chekecha toa mayenu,
Zungusha zungusha toa macheju,
Shika kamata shika kamata, mkamate tu,
Usirukie oversize, utapelekwa overtime,
Mshikaji umechoka, timeout!, achia ngoma,

Chorus
{Wa Jamila shilingi imemponza,
Kavaa don’t tachi, namwita anadengua} x2
{Si si si, simalikitu, se se se, segeju wa} x2
Chorus

Verse 2
Sandakalawe na mwenye kupata asijivunge,
Kama ni mkeo ah! mchunge ah! mzinge,
Mazichi wasimzonge,
Chanda kinene, hakiwezekani kuvishwa pete,
Kinataka vishwa kibwebwe cha kitenge,
Kwa mikiki kijidunge,
Simama dede lete makeke,
Minenguo kede tuonyeshe,
She utingishe, kama mkia wa kenge,
Zungusha msulupwete, akikukonyeza mvute,
Katikati msogeze ah! angalia asiwe,
Aliyemwacha mume wake, akafuata mdundiko,
Katikati ya burudani, utapewa mfuniko,
Usirukie oversize, utapelekwa overtime,
Mshikaji umechoka, timeout!, achia ngoma,

Chorus

{Mdundiko, mdundiko} x4

 

7. Kifimbocheza
Chorus
Cheza we!, cheza mwanangu,
Cheza we!, mbona  unanibania,
Na mimi ninataka watoto saba
Kifimbo cheza aa,  cheza we!
Kifimbo cheza aa,  cheza mwanangu
Kifimbo cheza aa, cheza we usinibanie
Mwenzio ninataka watoto saba,
Kifimbo cheza aa,  cheza we!
Kifimbo cheza aa,  cheza mwanangu
Kifimbo cheza,  cheza we mbona unanibania
Na mimi ninataka watoto saba,

Verse 1
Kiona mbali,
Nakuita kwani najua umetoka mbali,
Unaona mbali niambie usitake nilie,
Ma dot com wananilima na redio za mbao
Wanasema mimi ni gwa, nyoka niseye na Sumu, na Darda King niliwaambia
Aste aste ndio mwendo,nataka matendo ya maneno sikie usitake nicheke,
Pilipili iko shambani, imekuwashaje huko sokoni, chukueni time zenu nitakwenda ki Darda King,
Nikizuka kiwanja mimi nataka suuza roho,
Niondoe mawazo na uchovu wa siku nzima,
Khadija, Mwajuma, Rehema naye Neema,
Kwa mema, wamenizunguka mzichi sema,
Nasema, ila kwa herufi ndogo, navuta
Ndogo ndogo, kido kwani mimi sio mbaula,
Tuko kwenye mkoko, wote matumbo wazi
Kibandawazi, mwendo kama jahazi na
Wachumba kiti cha nyuma, nalonga,
Na sio natongoza inakuuma?, ongoza duka la
Dawa watakupa sumu ya panya, hunipendi
Pasuka sijali, kwani nimekosa nini na sasa
Umevimba kama chura, sawa sawa,
Jana umenitoa kwenye gazeti sura  ya mbele,
Kwamba mimi ni gumba na sina madhara,
Ahsante sana, ustaarabu umetushinda sasa
Ngoja tujaribu mbinde, nataka ubia na salama
Washikaji nisameheni, nataka mashemeji,
Wenyeji kwa wageni tukutane chumbageni,
Aheri ya mchawi, kuliko huyu dot com,
Ninafungua zip na ninaanza na dada yake,

Chorus

 

 

 

 

 

Verse 2
Mazichi tunaendeleza mambo kifimbocheza,
Tunatembeza bakora,
Hata ukipenda juu ya meza,
Hatuchagui mahala pa mechi
Wewe popote sema,
Tunapiga mikito ya kushindua, ukipendekeza
Nyamaza, utapakaza, makelele soo,
Chumba cha pili yuko braza,
Vumilia mpini, niendelee sukuma ndonga,
Utazoea tuu, mambo yatanoga,
Zungusha kiuno usilale kama boga,
Mechi ikiisha ndio tutapiga soga, ah! ah! ah!
Si unaona,
Mchezo utafika kilele mzichi nitapona
Nipate mtoto mwingine wa kike sura pina,
Ni lazima atoke bomba
Kama malikia wa Sheba,
Mtoto wa pili nimezaa na Mkikuyu,
Wa tatu Kalunde mama yake ni Mnyamwezi,
Atufigwe ndiye aliyenibebea wa nne,
Tano na sita mama yao ni Mmasai,
Damu ya mzichi ni kali kila inapogusa,
Kifimbocheza we!, kifimbocheza ah! ah! ah!,
Kifimbocheza ah! ah! ah!,

Chorus

Na wewe mpambe nuksi,
Unayepaka matope jina Langu kila siku,
Wewe endelea tu, yah! wewe Endelea tu, utashangaa mtoto wa saba,

Nazaa na demu wako, Yah! wewe endelea tu.

 

8. Walokole
Chorus
Lusifeli amechill x2
Walokole,  lusifeli amechill x4

Verse 1
Tazama walokole jinsi wanavyopigana,
Wenyewe kwa wenyewe mitutu wanashikiana
Ninaona  noma kusema nisiyotakiwa kuyasema
Wenye ujumbe wametema, jiwe limeinuliwa,
Msabato anamvuta shati Mlutheri
Unafanya nini bwana, Sabato ni Jumamosi
Jumapili unacheza amka usingizini,
Kilutheri ni theluthi tu ya nyota za angani,
TAG kampa loba EAG, unasemaje?
Unasema nini wewe, tuliza msuli,
Nikupe mistari iliyokaa kimshazali,
Kamata kipamfleti,
Natamani ungeona zali la Mbaptisti,
Alipomletea za kuleta Anglikana,
Ubatizo maji mengi, ndio njia pekee ya kuingia Mbinguni fungua sura ya kumi,
RC anasema Protestant, Revival, Pentecoste,
Na wasio na dhehebu, bwana wadogo,
Ninyi nyote mmetoka kwangu na mimi ni
Kama baba yenu, fuateni mienendo  yangu
Heshimu wakubwa zenu,
Kugawanya na kushinda ndio mbinu aliyotumia
Tofauti amewawekea kwa neno wanalotumia,
Wamesahau nani ni adui na nani wa kumpinga,
Wamebaki wanashikana mashati lusifeli amechill

Chorus
{Lucifeli amechill anavuta sigara
Anasema bila shaka Walokole nimewapata,
Lusifeli amechill anavuta sigara,
Anasema bila shaka Walokole wanajimaliza} x2

Verse 2
Kuna mambo ya mihadhara, sadaka, mhubiri,
Mtumishi, msaidizi, muimbaji, na mfuasi,
Na kutafisiriwa neno kwa kiasi na maombi,
Mzichi imenilazimu nitoe fungu la kumi,
Lusifeli angekitambua cha mtema kuni,
Wangesimama pamoja kama lilivyokuwa jeshi la Kirumi,
Kwa kuwa yeye sasa ni mtawala duniani,
Amewagawanya mafungu  ya makumi kwa makumi,
Nakumbuka enzi za kusali kwa Rozali,
Salamu Maria, ubatizo maji kidogo,
Komunio, kipaimara, na mafuta kupakwa,
Mpaka habari za ubatizo maji mengi,
Kutwa tangatanga ninakokwenda ndio kuzuri,
Nilipo sasa ndio safi, nilikotoka hakufai,
Kule kumepooza na pale kuna baridi,
Mti ulionyauka, matunda hauzai,
Tofauti zilitoka wapi, na kitabu ni kimoja,
Tofauti zilitoka wapi Mungu wao ni mmoja,
Wana jina moja, asili yao moja, siku ya mwisho Watahukumiwa na Mungu mmoja,
Kugawanya na kushinda ndio mbinu aliyotumia
Tofauti amewawekea kwa neno wanalotumia,
Wamesahau nani ni adui na nani wa kumpinga,
Wamebaki wanashikana mashati lusifeli amechill

Chorus


9. KituNaBoksi

Verse 1
Baragumu limelia,
Ujue kuna jambo lamgambo likilia,
Wanajeshi mguu pande, mguu sawa,
Heshima toa Mfalme ninaingia,
Ninatua, jijini Dar-es-Salaam,
Ninaleta salamu kutoka H-Town,
Ni muda mrefu umepita
Tangu nilipoondoka town,
Mazichi wengi wamenitoka lakini na get by,
Ni kitambo tangu mzichi nilipotoa nidhamu,
Wasanii wengi wamedondosha kalamu
Kwa mfalme hawana hamu, wanakumbuka,
Nilipowekewa mikono na wazee wenye hekima
Wakasema, adumu Mfalme Darda,
Nimekuwa, wa kutengenezea noti mtambo,
Kimwana niko kazini mapenzi sogeza kando,
Nimekuwa, chuma cha pua shoka la kibindo,
Nipe fifty feet, nakuja kama kimondo,
Kwenye barabara ya maisha spidi mia sitini,
Tairi likichomoka utapiga mia tatu sitini,
Jiwe kuu la pembeni, ukiniangukia oh ohh!

Chorus
{Sema na huo, mchanga wa macho,
Mzichi nilipotoka nilishakula kiapo,
Sema na huo, uji wa zege,
Karibu kama linaliwa la mtu jasho,
Sema na hilo, la chuma fagio,
Katikati ya foleni ya kiinua mgongo,
Sema na hilo, goli la kisigino,
KituNaBoksi sasa unaniona mikosi,} x2

Verse 2
King’ora kimelia,
Kimbia, jifiche chini ya meza ingia,
Majemedari tumeshuka mitaa tumekamata,
Mchakamchaka tumewakimbiza
Mpaka tumewapata,
Mchakamchaka chinja, alimselema khadija,
Hata chini wakitapatapa ,
Tunawakamata tunakita,
Hep hop, wamedata, ndege tunduni wamenasa,
Wame chokambaya, kushoto kulia ni midabwada
Unauliza, ndio kumbe sio,
Ukiambiwa unaziba masikio,
Country Boy mkononi paja la kuku na supu,
Umembulia kipapatio, afanalek,
Midundio iliyokwenda shule na miondoko ya kifalme, Afrika wanaipenda,
Bongo na genge, Ethiopia Tigrinya,
Coupe-decale Ivory Coast nimerusha,
Kizaramo zaramo, Mdundiko, nikapiga na Mapigo ya ki-Hamza Kalala kasimbago kabhoka,
Vinaelea ujue vimeundwa,
Mpishi ni Country Boy, nahodha ni Darda King,

Chorus

 

10. DardaKing
Chorus.
Da Darda Darda Darda, King x4

Mpenzi nakuomba, usoni nitazame
Ninapokuambia haya
Ni kwa nini wanataka tuachane,
Maneno maneno wanakupa,
Ninong’ono wana kunong’oneze,
Nong’ona nong’ona wanachonga 
Mpaka kwenye telephone,
Nataka tupendane wao wanataka tutengane
Tugombane tufarakane
Tupigane bunda ili watucheke,
Sijazaliwa jana na nina hekima za kifalme,
Ninaona watakachoona kesho,
Majaliwa yao, kwangu ni mapito,
Mimi ndio jabali, jabali lisilovunjika,
Ukiwa kifuani mwangu hakuna kusikitika,
Matatizo yako yote na maumivu yako yote,
Yaweke mikononi mwangu mami, jipumzishe,
Usikonde mpenzi wangu naam usihangaike
Himayani kwangu mimi ndio jibu mami usitishike
Pangua gia zote sweetie jiachilie,
Niweke gia zote beibe tuburudike,

Da Darda nakutazama nasikiliza usemacho
Da Darda walimwengu nimesikia wasemacho
Da Darda penzi lako ndio kitu nitamanicho
Da Darda nishikilie nitakushika mpaka mwisho,
Da Darda,
Je ningejisikiaje, kama ungependa mwengine,
Je ningejisikiaje, kama ungepata mwengine,
Mi ningejisikiaje, nisingekuwa na wewe
Mi ningejisikiaje, eeh
Na sijaona bado,
Wa kuniburudisha maishani mwangu,
Na sijaona bado,
Wa kunifurahisha maishani mwangu,
Na! bado, wa kumpiga busu kwa midomo yangu
Na! bado, wa kumpikia chakula kitamu,
Na! bado, wa kumkumbatia kwa mikono yangu,
Na! bado, kumfulia kwa vidole vyangu,

Chorus


11. Mwanamke
Chorus
Mwanamke atakupikia, Mwanamke atakufulia,
Mwanamke atakuhudumia,
Hata ukiumwa, mwanamke atakutibia,
Mwanamke anasikiliza, mwanamke anabembeleza,
Mwanamke anavumilia,
Ukichemsha, mwanamke atakukimbia,

Verse1
Rudi nyuma fikiri wakati ulipozaliwa,
Kila ukilia ng'aa maziwa umeshapewa,
Ukikasirika labda joto limemzidia,
Umecheua aah, tayari umesafishwa,
Rudi nyuma fikiri nyumbani ulivyolelewa,
Kila saa sita mchana msosi umeshapakuliwa,
Kabla ya kulala usiku hadithi utasimuliwa,
Malezi nyumbani, mwanamke anayajulia,
Umeshatoka mzigo, amekutua mzigo,
Pole na kazi mpenzi huku akikufungua vifungo,
Nguo kwenye maji sabuni taulo kiunoni bafuni,
Maji ya moto tayari ukitaka chai ready,
Ukilalamika ahh! maumivu ya mgongo,
Utapewa panadol kisha utakandwa mgongo,
Huwezi ondoka nyumbani usoni ukiwa na tongotongo,
Huduma nyumbani, mwanamke anazipatia,
Unapigwa butwaa asubuhi unapokurupuka,
Nguo zimepigwa pasi msosi mezani ameshaweka,
Watoto wako safi tayari shule kuwapeleka,
Alilala wa mwisho mh! saa ngapi aliamka,
Tai imekaa vibaya kiufundi inarekebishwa,
Ili usitoke vibaya na koti unavalisha,
Mbokoto tayari umeng'arishwa,
Mambo ya nyumbani mwanamke anayapatia,

Chorus

Verse 2
Miaka nenda rudi bado ana maintain,
Mambo yote ya nyumbani yeye ndio Captain,
Kama mwaka jana na juzi  bado yuko top ten
Hajashuka hadhi akikosa anaomba radhi,
Hizi huduma zote sasa kwako mazoea,
Hauthamini tena jinsi anavyojitolea,
Unasema hainogi tena ingawa imekolea,
Wacha mchezo, mwanamke atakukimbia,
Ah ah! umesusa hata hautaki tena,
Na kurudi kwako siku hizi ni usiku sana,
Habari za kazi poa na mchezo umekwisha
Hakuna maelewano ona unavyomsikitisha,
Akisema unabisha, akisema unabisha na kumkatisha
Mambo yakiharibika lawama unambebesha,
Ya leo kali pah! na kibao umemchapa,
Mambo ya nyumbani, mwanamke anavumilia,
Ameona haifai nyumba inakoelekea,
Anaumia jinsi ndoa inavyoteketea,
Ameona kwa wazazi kesi kuwapelekea,
Bado kichwa ngumu na wazazi unawakosoa,
Kumbuka ulikuwa chikonda, sasa umenenenepa,
Kumbuka ulikuwa kapela sasa ni baba Neema,
Amechoka anadai talaka unashituka,
Umeshacheza, mwanamke anakukimbia,

Chorus
Kibaya kwako, ni kizuri kwa mwenzio,
Wewe fanya mchezo tu na kile ulichonacho,
Tusije tukalaumiana bwana oh mimi sina bahati,
Oh nimelogwa, weka macho juu bwana

 

12. Mimi
Chorus
Mimi oh! ng'i ming'i ming'i ming'i oh! x4

Verse1
Darda King, Mfalme wa wafalme,
Katika ulimwengu wa kurap,
Wananipenda tena wananipa taji ya Almasi
Nijisikie kama mzazi wa midundo hii,
Namwaga radhi bila wasiwasi,
Nimetulia ndani ya BMW,
Vioo juu muziki juu napita juu juu,
Ninawatimulia vumbi wapambe nuksi
Wenye roho kama fisi ah! wanaoleta masimanzi,
Bongoflava, midundo ya kiswahili inafanya wabahili
Kumwaga mapesa nunua CD's,
Wajasilimali, kuchanja kadi nunua DVD's,
Waswahili wanasuuza roho zao namna hii,
Wapenda burudani wako nami kama hivi,
Wamenikubali, wanayarui mangoma ya Darda King
Ninang'ara kama rangi za viking, niite King,
Nimetoka Dar,  Tz, naminya Houston, Texas,
Na mazichi makini wanaosukuma Lexus,
Mineli midomoni, miguu ya kuku kiunoni,
Usiingie kwenye kumi sheria iko mkononi,
Ninayo ngome kali majeshi batalioni,
Nikilala wako nami tayari hatarioni,
Jogoo akiwika ninasaka milioni,
Jua likizama nahesabu bilioni,

Chorus

Verse 2
Unajua nini, mimi simpendi Darda King,
Sababu analeta za minato,
Mademu wanamtaka anawapiga kibuti,
Anawaambia nina mwali wakati yeye ni kapela
Ameleta mashitaka wameshikana mashati,
Kisa ni wangu wangu Darda, kumbe mzee umelala
Lalama unaona noma na unakula nyama choma,
Kizalizali na washikaji, huna mashemeji,
Wanaulilia wembe wape Darda King,
Changanya chapa cheki muda,
Kumbuka kutesa ni kwa zamu,

Hapana wangu sio hivyo, sio kila kikatishacho
Mbele yako halali yako, tawala macho yako,
Ukienda hivyo mja wangu kuna mdudu atakulamba
Atakuacha na kilo mbili, sikiliza maneno haya,
Vaa jinzi, funga zipu, tia kufuli, dunda zako mitaani
Bila wasiwasi na na, changudoa akikatisha
Usawa wako bana jicho mpige busu,
Mwambie nenda zako sina chako,
Akikushika shati,  wewe kaka twende gesti,
Mwambie hiyo noma labda tukafunge ndoa,

Chorus

 

 

 
Home  |  Media  |  Events  |  Photo  |  Contacts
Copyright © 2003 - 2007 Mfalme  |  Privacy Policy
n